Nafasi za Kusoma kupitia kwa Kuulizia (ILSs) ni rasilimali binafsishwa za kusoma kwa minajili ya wanafunzi, zikijumuisha maabara, programu tumizi, na aina nyingine yoyote ya nyenzo za midia mbalimbali. ILS hufuata mzunguko wa kuulizia Mizunguko ya kuulizia inaweza kutofautiana lakini mzunguko wa kimsingi wa Go-Lab hujumuisha maelezo ya Awamu, Uelewaji wa dhana, Uchunguzi, Hitimisho, na Mazungumzo. Nia ya ILS ni kuwapa wanafunzi fursa ya kuendesha majaribio ya kisayansi, wakiongozwa kupitia kwa mchakato wa kuulizia na kusaidiwa katika kila hatua.
Ukurasa huu unawasilisha ILS iliyoundwa na mwalimu au Go-Lab na/au timu ya Next-Lab (na mara nyingi katika uundaji-wenza), katika sehemu kubwa ya mikoa na kwa lugha nyingi. Unaweza kuunda ILS ukianzia maabara ya mtandaoni, lakini pia kunakili na kutumia ILS iliyopo kwa usaidizi wa jukwaa la uandishi la Go-Lab. Tembelea ukurasa wa Usaidizi pale ambapo utapata sampuli za video, vidokezo & ujanja, na makabrasha ya mtumiaji, yanayoelezea maana ya kufanya kazi kwenye jukwaa la uandishi la Go-Lab na namna ya kuchapisha ILS yako binafsi pindi inapokamilika.
Ikiwa unatafuta nafasi ya mtandaoni hasa yanafaa kwa somo la Benin, Kenya au Nigeria, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Makusanyo.
Kama utaichagua ILS kwa Portuguese, maelezo katika tovuti hii yatakuwa bado yameonyeshwa kwa Kiingereza, isipokuwa kama mwandishi wa ILS ametoa maelezo kwa Portuguese. Hata hivyo, ukibofya katika kitufe cha kuonyesha awali au kunakili ILS hadi Graasp, ILS itaonyeshwa kwa Portuguese, kama ilivyoundwa na mwandishi wa ILS.